×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wagonjwa 14 wa Covid-19 wafariki, wengine wawili wakihitaji uangalizi wa karibu

Wagonjwa 14 wa Covid-19 wafariki, wengine wawili wakihitaji uangalizi wa karibu

Watu wengine 968 wameambukizwa virusi vya korona nchini baada ya sampuli elfu sita mia sita na kumi kupimwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita na kufikisha jumla ya maambukizi kuwa elfu sabini na saba, mia tatu sabini na wawili.

Maambukizi ya leo ni sawa na asilimia kumi na nne nukta sita nne. Miongoni mwa walioambukizwa ni mtoto mdogo wa umri wa miezi miwili na mzee wa miaka tisini na mmoja. Aidha watu mia nane themanini na wanane ni Wakenya na themanini wakiwa raia wa kigeni.

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengine mia nne ishirini na mmoja, Mombasa tisini na mmoja, Kilifi themanini na wanane, Busia sabini na watatu, Kiambu hamsini na wanne, Kajiado thelathini, Nakuru ishirini na wawili, Uason Gishu Ishirini na mmoja, Machakos kumi na saba na Murunga vilevile Bungoma kumi na sita, Kirinyaga kumi na tatu, Makueni, Kisumu, Turkana, Tharaka Nithi na Meru kumi na mmoja kila kaunti, Marsabit wanane, Laikipia na Narok wanne kila kaunti, Kisii, Elgeyo Marakwet na Mandera watatu kila kaunti, Nandi na Kwale wawili kila kaunti na Kericho, Garissa, Wajir, Nyandarua na Trans Nzoia mmoja kila kaunti.

Katika takwimu za leo, Wizara ya Afya aidha imetangaza kuwa wagonjwa wengine mia moja hamsini na watano wamepona ambapo mia moja na kumi walikuwa wakihudumiwa nyumbani na arubaini na watano kwenye hospitali mbalimbali. Kwa jumla waliopona kufikia sasa ni elfu hamsini na moja, mia tano na saba.

Wakati uo huo wagonjwa wengine elfu moja, mia moja thelathini na mmoja wamelazwa kwenye hospitali mbalimbali huku wengine elfu saba ishirini na watatu wakiendelea kuhudumiwa nyumbani. Aidha wagonjwa wengine sitini na watatu wamelazwa kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi, thelathini na sita wakiwa kwenye vipumuzi, ishirini na sita wakiwa kwenye Oxijeni. Wengine sabini na wanne wamelazwa kwenye wodi za kawaida na wawili wakihitaji uangalizi wa karibu.

Hata hivyo wagonjwa wengine kumi na wanne wamefariki dunia na kufikisha jumla ya walioaga kuwa elfu moja, mia tatu themanini.