×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwili wa Mbunge wa Matungu, Justus Murunga kuzikwa tarehe 28 Novemba

Mwili wa Mbunge wa Matungu, Justus Murunga kuzikwa tarehe 28 Novemba

Mipango ya mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Matungu, Justus Murunga inaendelea nyumbani kwake hapa Jijini Nairobi sambamba na Mumias katika kaunti ya Kakamega, licha ya mahakama kutoa agizo la kusitisha shuhuli hiyo.

Kamati ya bunge inayoshughulikia mipango hiyo imesema mazishi hayo yamepangwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu, yaani Jumamosi ijayo.

Wanachama wa kamati hiyo ambao ni Cleophas Malala, Benjamin Washiali na Bernard Shinali wamefanya ziara nyumbani kwa marehemu Murunga, katika kijiji cha Makunda katika eneo la Matungu na Makutano katika eneo la Lugari na kukutana na familia yake.

Washiali amesema  mawakili wa bunge la kitaifa watakata rufaa dhidi ya  uamuzi wa kusimamisha mazishi na iwapo hawatafaulu basi wataahirisha hafla hiyo.

Ikumbukwe mahakama ilisitisha mipango ya mazishi ya marehemu Mutunga hadi kesi iliyowasilishwa na Agnes Wangui Wambiri anayejidai kuwa mkewe itakaposikilizwa na kuamulia

Hata hivyo, wajane wawili  wa marehemu Mbunge huyo ambao ni Christabel Jane na Grace Murunga wamesema hawamjui Agnes wala watoto wake wawili anaodai kuwa wa marehemu.