
Serikali imetakiwa kufungua shule na vyuo mapema kabla ya tarehe 4 Januari mwaka ujao jinsi ilivyotangazwa, ili kukabili visa vya ndoa na mimba za mapema miongoni mwa wasichana.
Akizungumza mjini Kapenguria, Gavana wa Pokot Magharibi Profesa John Lonyangapuo amesikitishwa na hali ambapo ya asilimia 29 ya mimba za mapema na asilimia 74 ya visa vya ukeketaji imerekodiwa katika kaunti hiyo pekee.
Kwa mujibu wa Lonyangapuo, hali hiyo imechangiwa na hali ambapo wanafunzi wamekuwa nyumbani kwa kipindi kirefu kutokana na Janga la korona.
Amemtaka Waziri wa Elimu Profesa Goerge Magoha kuwahusisha washikadau wote wa sekta ya Elimu ili kujadili kuhusu jinsi ya kurejelewa kwa masomo hara iwezekanavyo.