×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

DCI yawazuilia wanafunzi wengine 44 waliokamatwa wakiwa kwenye sherehe jijini Nairobii

DCI yawazuilia wanafunzi wengine 44 waliokamatwa wakiwa kwenye sherehe jijini Nairobii

Maafisa wa Idara ya Upelelezi wamewakamata wanafunzi wengine arubaini na wanne waliokuwa kwenye sherehe katika mtaa wa kifahari wa Mountain View hapa jijini Nairobi.

Katika taarifa DCI imesema wanafunzi hao pamoja na aliyeandaa sherehe hiyo wamekamatwa wakiwa na aina mbalimbali za pombe na dawa za kulevya.

Milicent Kithinji mwenye umri wa miaka arubaini na mmoja ndiye aliyeandaa sherehe hiyo na kwa sasa angali anahojiwa katika kituo cha polisi cha Dagoretti. Uchunguzi wa awali unaonesha kwamba wanafunzi hao ni wa kutoka jijini Niarobi, Kiambu na Machakos.

Miongoni mwa waliokamatwa ni wavulana ishirini na sita na wasichana kumi na wanane wa kati wa umri wa miaka kumi na minne na kumi na saba.

Wote ni wanafunzi wa shule za msingi na upili. DCI imeonya kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watu wanaowahadaa watoto wadgo.

Kwa sasa polisi wanaendelea kuchunguza tukio hilo wakitaka kubaini ni vipi wanafunzi hao walifika nyumbani kake. Kwa mara nyingine wazazi wameshauri kuwa makini na kufuatilia mienendo ya wanao hasa kwenye mitandao ya kijamii.

Tayari DCI imewasiliana na wazazi na watahojiwa ili saidia polisi kufahamu no vipi walivyotoweka nyumnai kwao bila wazazi kujua.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya DCI kusema kwamba wanalichunguza kundi linalotumia mitandao ya kijamii kuwahadaa wanafunzi wa shule kushiriki sherehe ambazo huendelea kwa siku kadhaa.

Ni juzi ambapo wasichana saba waliohadaiwa kwamba wangetafutiwa kazi waliokolewa na maafisa wa polisi baada ya kutoweka nyumbani bila wazazi kujua.

Share this: