×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sitisha mipango ya BBI, Mudavadi amwambia Rais Kenyatta

Sitisha mipango ya BBI, Mudavadi amwambia Rais Kenyatta

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kusitisha mipango ya kukusanya saini za kufanikisha kura ya maamuzi, kwa misingi kwamba shughuli hiyo itahatarisha maisha ya Wakenya kutokana na Janga la Korona.

Musalia, ambaye amekuwa miongoni mwa viongozi ambao wamekuwa wakikariri haja ya mapendekezo yenye utata katika BBI kuboreshwa ili kuleta mwafaka, amesema itakuwa vigumu kwa wananchi kuzingatia masharti ya kudhibiti Korona, wakati wa kukusanya saini zao.

Amerejelea ongezeko la vifo na maambukizi ya Virusi vya Korona katika siku za hivi karibuni nchini humu, akisema shughuli hiyo inafaa kuhairishwa hadi wakati viwango vya maambukizi vitakapopungua.

Aidha, Mudavadi amesema iwapo shughuli hiyo itaendelea jinsi ilivyopangwa, basi itailazimu serikali kuweka mikakati ya kuwawezesha wananchi kutia saini zao kwa njia ya mtandao, au kuhakikisha wananawa mikono na kuepuka mikusanyiko wakati wa mpango huo.

Kauli sawa na hiyo imetolewa na Aliyekuwa Mwenyeki wa Mamlaka ya Kudhibiti Matumizi ya Vileo na Mihadarati NACADA John Mututho, ambaye vilevile amesema serikali inafaa kufafanua jinsi itakavyofanikisha ukusanyaji saini za wananchi bila kuhatarisha maisha yao.

Share this: