×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Bado tunataka Mwafaka wa BBI, Naibu wa Rais asema

Bado tunataka Mwafaka wa BBI, Naibu wa Rais asema

Naibu wa Rais William Ruto ameendelea kukashifu mrengo wa Kinara wa ODM Raila Odinga kulazimisha Ripoti ya BBI kutekelezwa jinsi ilivyo kupitia kura ya maamuzi kabla ya kurekebisha mapendekezo yake tata.

Ruto amesema kwa mara nyingine kwamba kutumia nguvu kuwagawanya wananchi kuwa katika makundi mawili ya kuunga na kupinga ni kuhujumu umoja wa kitaifa.

Katika mtandao wa Twitter, Naibu wa Rais amesema,

" CONSENSUS was , is and will CONTINUE as our position. Pushing those with ALTERNATIVE or BETTER ideas to oppose BBI is raw arrogance which NEGATES any bridge - building efforts"

Aidha, Ruto amesema wanachama wa Jubilee hasa wabunge watafuata mwelekeo wa kuwanufaisha wananchi wala si manufaa ya viongozi wachache.

Wakati uo huo, Ruto ametuma risala za rambirambi kwa familia ya Dkt. Anthony Were Omolo ambaye amefariki dunia kutokana na Ugonjwa wa COVID-19.

Haya yanajiri huku Daktari Nira Patel ambaye ni mtaalamu wa meno akiwa mhudumu wa afya wa hivi punde kuaga dunia kufuatia COVI-19.

Daktari Nira alikuwa mke wa Mjasiriamali Pankaj Patel.

Kuaga dunia kwa 2 hao tarehe 21/ 21/ 2020 kunafikisha idadi jumla ya wahudumu wa afya ambao wamefariki  dunia kutokana na ugonjwa wa Covid 19 kuwa31, huku wengine 2, 366 wakiambukizwa Korona.