
Wakazi wa Wadi ya Ngarema kwenye Kaunti ya Isiolo wamesalimisha bunduki kumi waliozokuwa wakimiliki kinyume na sheria kufuatia oparesheni kali ya maafisa wa polisi.
Inaarifiwa oparesheni hiyo imekuwa ikiendelea kwa siku tano huku polisi wakisema kwamba wamekuwa wakiwatafuyta washukiwa waliowavamia maafisa wa polisi kwenye eneo la Makinya katika Barabara Kuu ya Isiolo-Meru.
Kamishna wa Isiolo Herman Shambia amesema usalama umeimarishw ahata zaidi huku akiwapongeza wakazi kwa kusalimisha bunduki hizo.
Shambi amesema Bunduki hizo zitachunguzwa kubaini iwapo zilitumika katika uvamizi huo dhidi ya maafisa wa polisi. Amesema iwapo itabainika kuwa zilitumika basi waliokuwa wakizimiliki watawajibishwa.
Ameapa kwamba oparesheni inayoendelea haitasitishwa hadi bunduki zote zinazomikiwa kinyume na sheria zimewasilishwa kwa maafisa wa usalama..
Bunduki zilizosalimishwa ni tatu aina ya AK47, moja aina ya G3 na nne aina ya M16. Aidha kulikuwapo na risasi mbili za G3 saba ya AK57 na tano z aina ya 303.