×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Daktari mwingine ameaga dunia kutokana na COVID-19

Daktari mwingine ameaga dunia kutokana na COVID-19

Sekta ya Afya imepata pigo jingine baada ya Daktari A J O Were kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid 19 leo asubuhi. Were alikuwa Rais wa Chama cha Afrika cha Madaktari wa kushughulikia waathiriwa wa matatizo ya figo.

Kifo cha dakirati huyo kinafikisha 31 idadi ya wahudumu wa afya ambao wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid 19 huku wengine elfu mbili mia tatu sitini na sita wakiambukizwa virusi vya korona.

Hayo yanajiri huku  wahudumu wa afya wakiendelea kuilaumu serikali kwa kupuuza hitaji la kuwapa bima ya afya wanapoambukizwa Virusi vya Korona.

Akizungumza katika uzinduzi wa Muungano wa Kitaifa wa Wahandisi wa Biometric NUBEK, Katibu wa Muungano wa Maafisa wa Kliniki George Gibore ametishia kutoa tangazo maalumu la mgomo siku chache zijazo iwapo matakwa yao hayatatekelezwa.

Gibore aidha amesisitiza kwamba wahudumu wa afya ambao ni wajawazito, wakongwe na wanaougua magonjwa hatarishi wanastahili kuruhusiwa kukaa kunyambani.

Tayari Muungano wa Madaktari, KMPDU umesema wanachama wake watagoma iwapo serikali haitatimiza matakwa yao.