×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya yawekeza pakubwa katika utafiti wa kisayansi, asema Rais Uhuru

Kenya yawekeza pakubwa katika utafiti wa kisayansi, asema Rais Uhuru

Rais Uhuru  Kenyatta amesema serikali yake itaendelea kuwekeza pakubwa katika Utafiti wa Kisayansi ili kukwamua taifa  kutokana na changamoto za kiuchumi na kufanikisha maendeleo.

Akizungumza hapa Jijini Nairobi kwa njia ya video wakati wa Makala ya Hamsini ya Maadhimisho ya Kimataifa kuhusu Fisiolojia ya Wadudu na Ekolojia ICIPE, Rais Kenyatta amesema serikali itaendelea kuwekeza zaidi katika mbinu za kisasa ili kubuni nafasi za ajira kwa Wakenya.

Kenyatta ameeleza haja ya vijana kutumia ubunifu wao ili kujiendeleza kimaisha kutokana na utafiti wa masuala ya wadudu, ufugaji, utunzaji mazingira na upanzi wa miche ili kufanikisha maendeleo.

Aidha, Rais amesema vijana Barani Afrika wana talanta mbalimbali ambazo zinafaa kuboreshwa Kisayansi ili kuafikia maendeleo.

Wakati uo huo, Mawaziri Raychelle Omamo wa Masuala ya Nchi za Kigeni na Mwanzake wa Kilimo Peter Munya wamesema sekta ya Kilimo itaimarika hata zaidi Barani Afrika kutokana na uvumbuzi wa utafiti wa Kisayansi.