×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

1048 waambukizwa korona, 19 wafariki

1048 waambukizwa korona, 19 wafariki

Kenya imefikisha idadi ya vifo vinavyotokana na Covid-19 kuwa elfu moja, mia tatu arubaini na tisa baada ya watu wengine kumi na tisa kufariki dunia kufuatia ugonjwa huo.

Haya yanajiri huku watu wengine elfu moja, arubaini na wanane wakiambukizwa virusi vya korona baada ya kupimwa kwa sampuli elfu nane, mia sita sitini katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Idadi ya leo inafikisha jumla ya walioambukiwa mchini kuwa watu elfu sabini na tano, mia moja tisini na watatu .

Miongoni mwa waliotangazwa leo kuambukizwa, elfu moja, kumi na wanane ni Wakenya huku thelathini wakiwa raia wa kigeni.

Aidha, mtoto mvulana wa mwaka mmoja na mkongwe wa miaka tisini ni miongoni mwa walioambukizwa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Afya imesema viwango vya maambukizi leo hii ni asilimia 12. 1 ikilinganishwa na asilimia 14. 4 ya jana.

Wakati uo huo, watu wengine mia tatu ishirini na sita wamepona Covid-19 na kufikisha idadi jumla ya waliopona nchini kuwa elfu hamsini, mia tisa themanini na wanne.

Miongoni mwa waliopona, mia mbili kumi na tisa walikuwa wakihudumiwa nyumbani, 107 wakiwa wale waliokuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali.

Kufikia leo watu elfu moja, mia moja kumi na wanne wamelazwa katika hospitali mbalimbali , elfu sita mia tatu thelathini na wawili wamewekwa karantini ya nyumbani.

Vilevile, watu hamsini na wawili wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi, ambapo ishirini na wanane wanatumia vipumuzi, ishirini na wanne wanatumia oxijeni, Sabini na mmoja wamelazwa katika wadi na wanatumia oxijeni, sabini wakilazwa katika wadi za jumla, huku mmoja akilazwa katika chumba cha wale wanaohitaji uangalizi wa karibu.