
Kamati ya Bunge ya Fedha na Mipangilio i katika Kaunti ya Lamu kukagua jinsi miradi ya serikali inavyoendelezwa na matumizi ya fedha za miradi hiyo.
Wanachama wa kamati hiyo wamekagua miradi ambayo imekamilika na ile inayotekelezwa huku mwenyekiti Gladys' Wanga akisema kwamba mradi wa pili wa bandari ya Lamu utakuza uchumi wa eneo hilo na taifa kwa jumla utakapo kamilika.
Naye Mbunge wa Lamu mashariki Stanely Muthama amesema ni wajibu wa serikali kutenga fedha zaidi ili kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali katika eneo hilo.
Amesema wakazi wanatatizika kusafiri kwa kutumia mashua.