×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Waiguru akwepa mtego wa faini katika seneti

Waiguru akwepa mtego wa faini katika seneti

Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru amekabiliwa na wakati mgumu kuieleza Kamati ya Uhasibu ya Seneti kuhusu ni kwa nini amekuwa akikosa kufika mbele yake mara kadhaa licha ya kutakiwa kufanya hivyo.

Wanachama wa kamati hiyo wamemtaka Waiguru kufafanua kwa nini aliamua kuhudhuria kongamano la magavana kujadili ripoti ya Mpango wa Upatanishi, BBI wakati ambapo alitakiwa kufika mbele ya seneti ili kujibu maswali kuhusu ukaguzi wa fedha za kaunti.

Samson Cherargei ni Seneta wa Nandi akiwa mwanachama wa kamati hiyo.

Gavana Waiguru hata hivyo, amejitetea akisema alituma ombi la kutaka tarehe hiyo kubadilishwa.

Imemlazimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Sam Ongeri kuingilia kati ili kumnusuru Waiguru dhidi ya kulipa faini ya shilingi laki tano.

Badala yake kamati hiyo imemuonya Waiguru dhidi ya kukosa kufika mbele yake tena, ikisisitiza kwamba itamchukulia hatua kali za kisheria.

Share this: