×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Asilimia 67 ya Wakenya haishughuliki katika vita dhidi ya ufisadi-EACC

Asilimia 67 ya Wakenya haishughuliki katika vita dhidi ya ufisadi-EACC

Mwenyikiti wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC Eliud Wabukala amesema asilimia 67 ya Wakenya haishughuliki kwa vyovyote na juhudi za kukabili ufisadi, huku asilimia 5. 8 pekee ikiripoti visa vya wizi wa fedha za umma.

Kwa mujibu wa utafiti wa EACC uliofanywa mwaka huu kwa kulinganisha na mwaka jana, Wabukala ametaja ukosefu wa ushirikiano baina ya wananchi na serikali kuwa mojawapo wa mianya inayotatiza juhudi za Kukabili ufisadi nchini.

Akirejelea hulka ya wananchi kushindwa kuwawajibisha viongozi na kuwachagua wanasiasa wenye maadili wakati wa uchaguzi, Wabukala amesema hali ya kutokuwapo kwa uwazi miongoni mwa watumishi wa umma kumechangia hali hiyo.

Aidha, amesema ufisadi unasalia kuwa changamoto kuu inayokabili taifa hili , hivyo basi kusisitiza haja ya wananchi kujitolea kushirikiana na taasisi za serikali ikiwamo EACC katika kufichua ufisadi.

Vilevile,  amewalaumu watumishi wa serikali kwa madai ya kushiriki katika njama za kuhitilafiana na ushahidi wa ufisadi hivyo kuhujumu mikakati ya kulinda rasilimali za umma

Wabukala amesema hayo kwenye hotuba ya video wakati wa kongamano la kuangazia maadili lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Strathmore hapa Jijini Nairobi.

Share this: