×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Bobi Wine aachiliwa kwa dhamana

Bobi Wine aachiliwa kwa dhamana

Mwaniaji wa urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine ameachiliwa kwa dhamana na Mahakama ya Iganga nchini humo.

Mahakama aidha imemwagiza Wine kuzingatia mwongozo wa kuzuia maambukizi ya korona wakati wa kempeini zake.

Haya yanajiri huku  Idadi ya watu ambao wamefariki dunia kutokana na makabiliano baina ya polisi na wafuasi wa Bobi Wine imefikia ishirini na wanane.

Ishirini na wanane hao wamefariki huku mia tano sabini na saba wakijeruhiwa baada ya ghasia kuzuka Bobi Wine alipokamatwa na polisi kwa madai ya kupuuza mwongozo wa kuzuia maambukizi ya korona wakati wa kampeini zake.

Hata hivyo, wafuasi wake wanasema alikamatwa kutokana na sera zake za kupinga uongozi dhalimu wa rais Yoweri Kaguta Museveni.

Polisi wamezingira mji wa Kampala wakiwakabili waandamanaji wanaopinga tukio la kunaswa kwake siku ya Jumatano alipokuwa akiendesha kampeini zake Mashariki ya Uganda

Msemaji wa Polisi nchini Uganda Fred Enanga amesema waandamanaji wamekuwa wakijihusisha na uvunjaji wa sheria na kuwakabili wasiokuwa wafuasi wa Chama cha Bobi Wine, National Unity Platform, NUP.

Uganda inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu Januari tarehe 14 mwaka ujao huku Wine mwenye umri wa miaka thelathini na minane akionekana kuwa mshindani mkuu wa Rais Museveni mwenye umri wa miaka sabini na sita ambaye analenga kuzidisha uongozi wake baada ya kuwa uongozini kwa muda wa miaka arubaini.

Share this: