
Mili yote kumi ya watu waliozama katika Ziwa Victoria baada ya mashua waliokuwa wakisaria kusama imeopolewa.
Maafisa wa Kenya Coast Guards wamefanikisha shughuli ya kuitafuta mili hiyo. Mkuu wa polisi wa eneo la Nyanza Karanja Muiruri amesema mili iliyoopolewa inakabidhiwa familia ili kuwapa nafasi kuanza mipango ya mazishi.
Mashua hiyo iliyokuwa imewabeba watu ishirini, mahindi na ndizi kutoka taifa jirani ya Uganda ilizama muda mfupi tu kablaya kutia nanga siku ya Jumatano wiki hii .
Watu kumi waliokolewa huku wengine kumi wakizama.