×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Magavana kutoa taarifa kuhusu hali ya kaunti wakati huu wa korona

Magavana kutoa taarifa kuhusu hali ya kaunti wakati huu wa korona

Baraza la Magavana leo hii linatarajiwa kufanya kikao na wanahabari kuzungumzia masuala kadhaa yanayoziathiri kaunti katika vita dhidi ya janga la korona.

Miongoni mwa masuala hayo ni hali ya wahudumu wa afya katika kaunti walioko mstari wa mbele kukabili korona, utayarifu wa kaunti katika kuendelea kukabili janga la korona na usambazaji wa fedha hadi kwenye kaunti kutoka kwa serikali ya kitaifa.

Kikao cha leo kitafanyika baada ya kingine cha jana ambapo Baraza la Magavana lilikutana kujadili masuala kadhaa kuhusu janga hilo kabla ya kuafikia uamuzi wa kufanya kikao kingine leo hii.

Kufikia sasa kaunti mbalimbali zimeweka mikakati ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona ambavyo vimesababisha vifo huku maafisa mbalimbali wa kaunti wakiendelea kutibiwa baada ya kuambukizwa.

Katika kipindi cha mwezi mmoja pekee, wawakilishi wadi watano wamefariki dunia katika visa vinavyohusiswa na korona. Wawakilishi wadi wawili wamefariki dunia kwenye Kaunti ya Nakuru, Mombasa mmoja sawa na Kisii na Uasin Gishu.

Hapo jana Serikali ya Kaunti ya Murang'a ilianza shughuli ya kupuliza dawa ya kuua viini kwenye masoko na maeneo mengine ya umma.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya katika Kaunti ya Murang'a Joseph Mbai, masoko 144 yanatarajiwa kupuliziwa dawa katika kipindi cha miezi mitatu ijayo. Kaunti nyingine ambazo pia zimeweka mikakati mbalimbali ya kukabili korona kufuatia ongezeko la maambukizi ni Meru, Nakuru, Kilifi miongoni mwa nyingine.

Share this: