×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Madaktari hulazimisha kufanya kazi licha ya kukiri kwamba wana korona-Mwachonda

Madaktari hulazimisha kufanya kazi licha ya kukiri kwamba wana korona-Mwachonda

Imebainika kwamba madaktari wanaoambukizwa virusi vya korona bila kuonesha dalili zozote wamekuwa wakilazimishwa kuendelea  kufanya kazi hali inayowahatarisha  maelfu  ya Wakenya.

Hayo yamesemwa na Chama cha Madaktari nchini KMPDU. Katibu Mkuu wa Chama hicho Chibanzi Mwachomnda amesema hali hiiyo imechangiwa na kuongezeka kwa idadi ya wanaoambukizwa korona na idadi ndogo ya madaktari hasa katika hospitali za umma.

Mwachonda ameieleza kamati ya Seneti ya Afya kwamba kando na hayo matatizo mengine yanayowakumba wahudumu wa afya kama vile mazingira duni ya kufanyia kazi, ukosefu wa marupurupu na bima ya afya wanapougua yanaathiri utendakazi wao.

Ameonya kwamba iwapo masuala hayo hayatashughulikiwa basi wataendelea na mgomo wao jinsi walivyopanga.

Kulingana na Wizara ya Afya kufikia sasa kuna wahudumu wa afya elfu mbili mia tatu hamsini na wawili ambao wameambukizwa korona nchini huku, thelathini wakifariki dunia.

Kenya ina jumla ya watu elfu sabini na nne, mia moja arubaini na watano walioambukizwa korona na wengine elfu moja, mia tatu thelathini wakifariki dunia.

Share this: