×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Tutaendelea na mgomo iwapo masuala yetu hayatazingatiwa-Madaktari

Tutaendelea na mgomo iwapo masuala yetu hayatazingatiwa-Madaktari

Madaktari wamesisitiza kwamba wataendelea na mgomo wao jinsi walivyopanga iwapo maslahi yao hayatashughulikiwa.

Wakizungumza walipofika mbele ya kamati ya seneti ya Afya,  viongozi wa vyama vya kutetea maslahi ya wahudumu wa afya wamesema kwamba wanahofia maisha yao hasa kufuatia kuendelea kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya korona.

Katibu Mkuu wa Chama cha madaktari nchini Chibanzi Mwachonda, amesema madaktari hawana motisha ya kufanya kazi kutokana na mazingira duni, ukosefu wa vifaa vya kujikinga, bima ya matibabu na marupurupu kipindi hiki cha korona.

Chibanzi ameliomba Bunge kuharakisha mchakato wa kisheria kuhakikisha kwamba Tume ya Huduma za Wahudumu wa Afya inabuniwa ili kuyashughulikia maslahi yao akisema wamehangaika kwa muda mrefu hasa tangu sekta hiyo muhimu kugatuliwa.

Wakati uo huo,  amesema baadhi ya serikali za Kaunti kama vile Kirinyaga na Laikipia zimekuwa zikiwadhulumu madaktari kwa kuwafuta kazi wanapolalamikia maslahi yao.

Amesema haifai serikali za kaunti kutumia tofauti ambazo zimekuwapo baina yao na madaktari kwa muda mrefu kuendelea kuwadhulumu.