×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Duale awasuta wabunge waliobubujikwa machozi wakiwatetea madaktari

Duale awasuta wabunge waliobubujikwa machozi wakiwatetea madaktari

Mbunge wa Garissa Mjini, Aden Duale amewasuta wabunge wanachama wa Kamati ya Afya kwa kutiririkwa na machozi wakati walipokuwa wakimhoji Katibu Mkuu wa Muungano wa Madaktari, KMPDU Chibanzi Mwachonda na wawakilishi wengine katika sekta ya afya.

Kwa mujibu wa Duale, wabunge hao waliahibisha bunge lote hasa ikizingatiwa wana jukumu la kuliwakilisha katika kamati hiyo.

Duale amesikitishwa na jinsi wabunge hao walivyoonesha udhaifu wao mbele ya wakuu wa madaktari walipokuwa wakielezea jinsi serikali imewatelekeza msimu huu wa korona. Duale amesema kikatiba, kamati hiyo inaruhusiwa kumuagiza Waziri wa Afya na mwenzake wa Fedha vilevile wakuu wengine katika sekta ya afya kufika mbele yake ili kuwajukumisha. Pia amesema wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha bajeti inatengwa ili kuwalipa madaktari mishahara na marupurupu wala si kulia katika vyombo vya habari.

Kauli yake inajiri siku moja tu baada ya Mbunge wa Seme, James Nyikal na wenzake wa kamati hiyo ya afya kububujikwa na machozi walipofahamishwa kuhusu masaibu wanayopitia wahudumu wa afya.

Akizungumza wakati wa vikao vya alasiri hii, Duale pia amewashtumu baadhi ya wabunge kufuatia pendekezo la kutaka matibabu maalumu, wakati ambapo Wakenya wanapitia changamoto nyingi wakati huu wa korona. Amesema hakuna aliye na hitaji muhimu kuliko mwingine.