
Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha amesema kalenda mpya ya elimu itazingatiwa ili kuhakikisha wanafunzi hawapotezi mwaka mwingine wa masomo. Akizungumza katika Shule ya Msingi ya Kasawa kwenye Kaunti ya Kisumu, Magoha amesema wanaoipinga kalenda hiyo wanafaa kupendekeza nyingine badala ya kupinga tu. ikumbukwe Wizara ya Elimu imeagiza kufunguliwa kwa taasisi zote za elimu Januari 4 mwaka ujao.
Waziri Magoha aidha amesema shughuli ya utengenezaji wa madawati kwa kima cha shilingi milioni 1.9 imefaulu pakubwa na tayari yameanza kusambazwa kwenye shule mbalimbali nchini.
Waziri Magoha aidha amesisitiza kauli yake kwamba hakuna mwanafunzi anayestahili kufukuzwa shuleni kwa ukosefu wa karo huku akiwashauri wazazi wenye uwezo wa kuwalipia wanao karo kufanya hivyo.