×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

1459 waambukizwa korona, 17 wafariki

1459 waambukizwa korona, 17 wafariki

Kwa mara ya kwanza Kenya imepima sampuli ya juu zaidi tangu kuripotiwa kwa virusi vya korona nchini. Katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita, sampuli elfu kumi, mia moja arubaini na sita zimepimwa ambapo watu elfu moja, mia nne hamsini na tisa wameambukizwa virusi vya korona.

Idadi hii inafikisha jumla ya maambukizi nchini kuwa watu elfu sabini na wanne, mia moja arubaini na watano.

Miongoni mwao, elfu moja, mia nne kumi na tisa ni Wakenya huku arubaini wakiwa raia wa kigeni. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Afya imesema watu mia nane thelathini na watano ni wanaume, wanawake wakiwa mia sita ishirini na wanne.

Aidha, mtoto mdogo wa miezi minne na mkongwe wa miaka tisini na saba ni miongoni mwa walioambukizwa leo hii.

Viwango cha maambukizi leo hii ni asilimia 14.4 kulinganishwa na jana ambapo vilikuwa asilimia 17.2.

Habari njema ni kwamba watu mia saba themanini wamepona ugonjwa wa Covid-19 na kufikisha jumla ya waliopona kuwa watu elfu hamsini, mia sita hamsini na wanane kote nchini.

Mia sita tisini miongoni mwao walikuwa wakihudumiwa nyumbani huku tisini wakiwa wale waliokuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini.

Hata hivyo, watu wengine kumi na saba wamefariki dunia kufuatia ugonjwa huo. Kwa sasa idadi ya vifo nchini imefikia elfu moja, mia tatu thelathini.

Wakati uo huo, jumla ya watu elfu moja, mia moja kumi na sita wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini. Elfu sita mia mbili thelathini wawili wamewekwa karantini ya nyumbani.

Wengine hamsini na tisa wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi, ishirini na saba wanatumia vipumuzi, themanini na watatu wakitumia oxijeni na wengine kumi na sita wakilazwa katika vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu.

Share this: