
Rubani mmoja amefariki dunia baada ya ndege ya Shirika la Huduma za Wanyamapori, KWS aina ya helikopta kuanguka katika eneo la Isinya kwenye Kaunti ya Kajiado.
Mkuu wa Polisi wa Isinya, Kinyua Mugambi amesema ndege hiyo ilikuwa na mtu mmoja pekee. Chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo bado hakijabainika.