×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Reggae yasimamishwa kwa muda

Reggae yasimamishwa kwa muda

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Mvutano kuhusu baadhi ya mapendekezo katika Ripoti ya BBI umesababisha kuahirishwa kwa hafla ya uzinduzi wa ukusanyaji wa saini milioni moja ili kufanikisha mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho.

Shughuli ya uzinduzi huo, ilitarajiwa kufanyika Ijumaa ikiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na mshirika wake Raila Odinga.

Hatua ya kuahirishwa kwa hafla hiyo, imeafikiwa kufuatia kikao baina ya Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Ruto, wandani wake na baadhi ya viongozi wakiwamo wa kidini wamekuwa wakishinikiza masuala yanayoibua utata katika ripoti hiyo kurekebishwa huku Odinga akisema kwamba hakuna nafasi zaidi ya marekebisho.

Muda mfupi tu baada ya kikao hicho, Kamati ya Kitaifa inayoshughulikia BBI ilitoa taarifa ikisema kwamba kuahirishwa huko kumechangiwa na kuchelewa kuchapishwa kwa mswada wa marekebisho ya katiba.

Viongozi wa kamati hiyo, Junet Mohamed na Dennis Waweru wamesema umma utajulishwa kuhusu siku ambayo ukusanyaji wa saini hizo itazinduliwa. Uchapishaji wa msawada huo tayari umeanza.

Kiongozi wa Chama cah ANC Musalia Mudavadi amesema kwamba kuna haja ya kuwapo kwa maafikiano baina ya viongozi, akisema kuahirishwa kwa kikao cha leo kunatoa nafasi ya mazungumzo.

 

Haya yanajiri huku wandani wa Ruto wakipongeza mwafaka baina yake na Kenyatta kuhusu kuahirishwa kwa shughuli hiyo.

 

Seneta wa Elgeiyo Marakwet Kipchumba Murkomen amempongeza Kenyatta kwa kusikiliza malalamiko ambayo yamekuwa yakiibuliwa. Murkomen amesema hatua hiyo sasa itafanikisha kuwapo kwa maafikiano kuhusu BBI.

Mbunge wa Soy Caleb Kositany amesema kwamba kwa sasa Kenyatta amechukua uongozi kamili wa BBI na kuwa Wakenya wanatarajia Kenyatta, Odinga na Ruto watashughuliakia masuala ambayo yanaibua utata.

Kositany aidha amesema kwa sasa ngoma ya reggae imesimama huku akihusisha hali hiyo na maombi.