×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 11 wameaga dunia huku 957 wakiambukziwa korona

Watu 11 wameaga dunia huku 957 wakiambukziwa korona

Idadi ya watu wanaofariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya korona inazidi kuongezeka humu nchini huku watu wengine kumi na mmoja zaidi wakiaga dunia.

Kumi na mmoja hao wamefariki dunia katika kipindi cah saa ishirini na nne zilizopita hivyo kufikisha idadi jumla kuwa elfu moja mia tatu kumi na tatu baada ya kumi na mmoja zaidi kuaga dunia katika saa ishirini na nne zilizopita.

Wakati uo huo watu wengine mia tisa hamsini na saba  wameambukizwa virusi vya korona katika kipindi hicho. Idadi hii imetokana na sampuli elfu tano mia tano hamsini na tisa kumaanisha kwamba viwango vya maambukizi nchini ni asilimia 17.2.

Idadi jumla ya maambukizi nchini sasa ni elfu sabini na mbili mia sita themanini na sita.

Walioambukizwa mia tisa na wanane ni Wakenya na arubaini na tisa ni raia wa Kigeni. Kaunti ya Nairobi leo hii ndiyo pekee imerekodi visa zaidi ya mia tatu huku kaunti nyingine zikiwa na chini ya visa sitini.

Walioathibitishwa Nairobi ni watu  mia tatu sitini na wanane, ikifuatwa na Nyeri na watu hamsini na watatu, arubaini na moja Kitui, Kiambu arubaini, Kisumu thlathini na saba, Nyandarua thelathini na watano, Mombasa tehalthuini na wanne sawa na Uasin Gishu Kisha kakamega thelathini na watatu.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema watu elfu mbili mia sita kumi na sita wamepona na kufikisha jumla kuwa elfu arubaini na tisa mia nane sabini na nane.

Kwa sasa kuna wagonjwa elfu moja mia moja tisini na mmoja wa COVID -19 ambao wamelazwa katika hospitali mbalimbali, hamsini na wanane wakiwa ICU, elfu lfu sita wanahudumiwa nyumbani.

Wahudumu wa afya waliambukziwa korona ni elfu mbili mia tatu sitini na tisa  huku thelathini wakifariki dunia kufikia sasa.

Hayo yanajiri huku serikali ikiendelea kusisitiza gharama ya juu ya matibabu ya virusi vya korona. Mapema leo Kaimu Mkurugenzi wa Matibabu wa Wizara ya Afya Daktari Patrick Amoth amesema kwamba itamgahrimu mgonjwa asiye na dalili za covid-19 shilingi elfu ishirini na moja kuhudumiwa kwa siku iwapo atalazwa hospitalini, huku aliye na dalili anaweza kutumia shilingi elfu hamsini na moja mia sita themanini na nne kwa siku kuhudumiwa hospitalini.