×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Washukiwa 3 wa ulanguzi wa watoto watasalia korokoroni hadi Alhamisi

Washukiwa 3 wa ulanguzi wa watoto watasalia korokoroni hadi Alhamisi

Afisa Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya Mama Lucy Emma Mutio, Msimamizi wa Huduma wa Hospitali hiyo Regina Musembi na Mfanyakazi mmoja wa Jamii Fred Leparan waliokamatwa kufuatia ulanguzi wa watoto watasalia korokoroni kwa siku moja zaidi.

Watatu hao wamefikishwa mahakamani baada ya kukamatwa mapema leo japo hawakusomewa mashtaka baada ya Idara ya Upelelezi kuomba muda zaidi kukamilisha uchunguzi.

Afisa wa Uchunguzi wa DCI Wanga Masaki amemwambia Hakimu Mkuu Benard Ochioi kwamba washukiwa walikamatwa kufuatia taarifa waliyoipata kutoka kwa Leparan kuhusu kuhusika kwao katika baishara hiyo haramu.

Aidha Masaki ameieleza mahakama kwamba wana imani kuwa kuna kundi na watu wengine zaidi wanaohusika na biashara hiyo haramu na wataendelea kutafutwa.

Hata hivyo washukiwa hao kupitia wakili wao Danston Omari wamepinga kuzuiwa kwao wakisema Mutio alianza kufanya kazi katika Hopsitali hiyo ya Mama Lucy siku kumi zilizopita, awali alikuwa akihudumu katika Hospitali ya Mbagathi. Aidha amesema hakuna ushahidi uliowasilishwa kuonesha kuwa iwapo wangeachiliwa wangewaingilia mashahidi jinsi upande wa utetezi ulivyodai.

Uamuzi kuhusu iwapo wataachiliwa kwa dhamana au la utatolewa kesho. Wa sasa wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa.

Hayo yanajiri huku serikali ikubuni jopo maalum kuchunguza sakata ya ulanguzi wa watoto nchini.

Hatua hii inafuatia taarifa iliyopeperushwa kupitia Shirika la BBC ambapo maafisa kadhaa walionekana wakishirikiana kufanikisha uuzaji wa watoto kwa bei rahisi jijini Nairobi na maeneo mengine nchini

Waziri wa Leba na Masuala ya Kijamii Simon Chelugui amesema jopo hilo linawahusisha maafisa wa vitengo mbalimbali vya serikali.