×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Pfizer imesema chanjo yake dhidi ya korona imefanikiwa kwa 95%

Pfizer imesema chanjo yake dhidi ya korona imefanikiwa kwa 95%

Matumaini yanazidi kuongezeka kuhusu kupatikana kwa chanjo ya virusi vya korona.

Ripoti ya hivi punde ya kampuni ya Pfizer inaonesha kwamba chanjo yake inayoendelea kufanyiwa majaribio imefanikiwa kwa asilimia 95.

Chanjo hiyo inayotengenezwa akwa ushirikiano na kampuni ya Ujerumani ya BioNTech aidha inasemekana kuwa na uwezo wa kuwakinga watu wenye umri mkubwa dhidi ya COVID-19.

Ripoti hii inajiri wiki moja baada ya kampuni iyo hiyo kutoa ripoti nyingine iliyoonesha kwmaba imefanikiwa kwa asiliia 90.

Kampuni hiyo sasa imesema katika siku chache zijazo itaomba idhini kutoka kwa mamlaka ya chakula na dawa nchini marekani ili ianze kutumika wakati wa dharura. Wakati uo huo, data hiyo ya hivi punde itawasilishwa katika mashirika mengine kote duniani.

Awali kampuni Pfizer imesema inapanga kutengeneza dozi milioni hamsini za chanjo hiyo ifikiapo mwisho wa mwaka huu na nyingine bilioni 1.3 ifikiapo mwisho wa mwaka ujao.

Jumatatu wiki hii kampuni ya Moderna inayotengeneza pia chanjo cha virusi vya korona ilitoa ripoti yake iliyooneha kwamba imefanikiwa kwa asilimia 94.5.