×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wabunge walia kufuatia hali ngumu ya wahudumu wa afya

Wabunge walia kufuatia hali ngumu ya wahudumu wa afya

Hali isiyo ya kawaida imeshuhudiwa bungeni ambapo wabunge wamelia walipofahamishwa kuhusu hali mbaya ya wahudumu wa afya ambao wametelekezwa na serikali wakati huu wa maambukizi ya korona.

Wabunge hao wanachama wa Kamati ya Afya wakiwamo James Nyikali, Sarah Korere na Joyce Emanikor wamebubujikwa na machozi walipoelezwa kwamba madaktari wamekuwa wakihudumu bila malipo, mazingira duni na ukosefu wa bima ya afya.

Kamati hiyo aidha imesikitishwa na taarifa kwamba daktari mmoja katika Kaunti ya Lamu alifutwa kazi kufuatia kuugua ugonjwa wa Covid -19 huku Gavana Fahim Twaha akipuuza madai hayo na kusema anajitafutia umaarufu.

Kamati hiyo imekuwa ikisikiliza malalamiko ya wahudumu wa afya ambao wamekuwa wakigoma wakilalamikia kutolipwa mishahara na marupuru, kutopandishwa vyeo na mazingira dunia ya kufanyia kazi.

Hali hii imejiri huku serikali ikiahidi kwamba wahudumu wa afya wataanza kupewa bima ya afya wanapoathirika kutokana na korona.