
Kadi za huduma namba zitaanza kukabidhiwa waliosajiliwa tarehe mosi Desemba.
Kwa mujibu wa Waziri wa Teknolojia na Mawasiliano, Joe Mucheru, shughuli ya utoaji kadi hizo itaendelea huku kufikia mwisho wa mwaka ujao, kadi hiyo ikisalia kuwa ya pekee yenye ya kumtambulisha Mkenya anaposaka huduma za umma badala ya kitambulisho kuanzia tarehe 12 mwaka ujao.
Hivi leo Mucheru na mwenzake wa masuala ya ndani Dkt Fred Matiang'i wanaongoza afla za uhamasisho katika Kaunti za Machaos na Kiambu mtawalia. Hatua hii inafuatia kuapishwa kwa Kamishna wa Data ambaye ni Immaculate Kassait.