×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya hupoteza takribani ekari 5 ya misitu kila siku

Kenya hupoteza takribani ekari 5 ya misitu kila siku

Kenya hupoteza takribani ekari tano ya misitu kila siku kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu vilevile mikasa mbalimbali kwenye mbuga za wanyama.

Akizunga kwenye warsha na wanahabari kuhusu mazingira, Mwakilishi Wa Shirika la Maendeleo la Umoja Wa Mataifa Nchini Walid Badawi, amesema hali hiyo imeendelea kuirejslesha nyuma Kenya katika juhudi zake za kuafikia asilimia kumi ya misitu nchini. Aidha amesema UNDP inaendelea kushirikiana na Wizara ya inayohusika ili kuhakikisha suala hilo linadhibitiwa.

Aisha akitoa baadhi ya takwimu za hali ya misitu nchini, Katibu katika Wizara ya Mazingira Chris Kiptoo amesema Kaunti ya Nyeri ndiyo ambayo ina asilimia kubwa ya misitu kwa kuwa na 38% ikifuatwa na Jason Gishu kwa 37.5% kisha Lamu kwa takribani asilimia 34.

Hata hivyo Smetana kaunti ya za Migori, Kisumu na nyingine za Eneo la Nyanza kuwa zilizo na chini ya asilimia mbili ya misitu. Kiptoo aidha  amewahimiza washkdau kuendelea kushrikiana katika kiboresha hali ya misitu nchini.

Kwa ipande wake Shirika la Kihifadhi Misitu KFS limesisitiza haja ya kutekelezwa kwa sheria ya uchomaji makaa. Aidha limesema kuwa likishirikiana na Wizara ya Mazingira linalenga kupanda niche zaidi ya bilioni mbili kufikia mwaka 2022, mpango ambao UNDP imesema itashorikiana kuhakikisha unatekelezwa.