
Watu kumi wameripotiwa kufariki dunia baada ya mashua waliokuwa wameabiri kuzama katika Ziwa Victoria eneo la Usenge, Kaunti ya Siaya.
Mkuu wa Polisi eneo hilo Francis Kooli amesema kwamba mashua hiyo ilikuwa ikisafirisha mizigo kutoka Uganda na ilikuwa na abiria 20. Kufikia sasa, ni miili 10 iliyoopolewa kutoka ziwa hilo huku watu wengine kumi wakiwa hawajulikani waliko.
Aidha, Kooli amesema kwamba shughuli za kuwatafuta waliozama imetatizwa na mawimbi makali yanayovuma.