×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu wengine 925 waambukizwa korona nchini Kenya

Watu wengine 925 waambukizwa korona nchini Kenya

Kenya imerekodi asilimia 16.6 ya maambukizi ya virusi vya korona leo hii baada ya watu mia tisa ishirini na watano kuthibitishwa kuambukizwa kutokana na sampuli elfu tano mia tano hamsini na tisa zilizopimwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita. Jinsi

Miongoni mwa watu  mia tisa ishirini na watano waliothibitishwa kuambukizwa,  mia nane tisini na wawili ni raia wa Kenya huku thelathini na wawili wakiwa wa mataifa ya kigeni. Wanaume walioambukziwa ni mia tano hamsini na sita huku wanawake wakiwa mia tatu sitini na tisa. Mtu mchanga zaidi aliyeambukizwa ana umri wa miezi mitano na mzee zaidi tisini na miwili.  Idadi jumla ya maambukizi nchini sasa imefikia elfu sabini na moja, mia saba ishirini na tisa  idadi jumla ya watu walioambukizwa nchini. 

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa idadi ya maambukizi ambapo watu mia tatu hamsini na wanane wamethibitishwa kuambukizwa, Kiambu mia moja na wawili, Mombasa hamsini na tisa ikufuatiwa na Nakuru watu thelathini na tisa.

Aidha ni habari njema baada ya watu elfu moja na kumi na wanane kupona virusi vya korona ambapo mia nane hamsini ni wale waliokuwa wakihudumiwa nyumbani huku mia moja sitini na wanane wakiwa waliokuwa hospitalini. Idadi jumla ya waliopona sasa imefikia elfu arobaini na nne, mia mbili sitini na wawili.

Hata hivyo watu 15 wamefariki dunia katika kipindi cha saa ishirini na nne na kufikisha idadi ya waliofariki kuwa elfu moja, mia tatu na wawili.

Kufikia sasa watu elfu moja mia mbili thelathini na saba wanahudumiwa katika hospitali mbalimbali nchini na wengine elfu sita mia mbili hamsini na saba wakihudumiwa nyumbani.  Watu 62 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi, 26 miongoni mwao wamewekewa vipumuzi huku 32 wakiwekewa hewa ya oxjeni. Aidha 23 wako katika vyumba vya wanaohitaji uangalizi wa karibu, HDU.

Wahudumu wa afya ambao wameambukizwa kufikia sasa ni 2,352 ambapo  elfu moja mia moja sabini  na saba ni wanaume huku wanawake wakiwa elfu moja mia moja sabini na watano. Jumla ya wahudumu wa afya 30 wamefariki dunia kufikia sasa.

Hayo yanajiri huku Serikali ya Kaunti ya Meru imesitisha huduma zake hadi Disemba 7 kufuatia ongezeko la maambukizi ya virusi vya korona. Gavana Kiraitu Murungi ametoa mfano wa kitengo kimoja cha kaunti ambacho wafanyakazi kumi na wawili wameambukizwa korona miongoni mwa kumi na sita. Kitengo hicho hufanya kazi kwa katibu na ofisi ya gavana.