×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Zaidi ya wakimbikizi elfu thelathini wametorokea nchini Sudan kutoka Ethiopia

Zaidi ya wakimbikizi elfu thelathini wametorokea nchini Sudan kutoka Ethiopia

Zaidi ya wakimbikizi elfu thelathini wametorokea nchini Sudan kutokana na mapigano katika Eneo la Tigray nchini Ethiopia.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbikizi UNHCR takribani wakimbizi elfu nne wamekuwa wakitorokea nchini Sudani tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika eneo hilo.

Msemaji wa UNHCR Babar Baloch ameviambia vyombo vya habari kwamba takribani wanawake na watato elfu kumi na nne mia tano ni miongoni mwa wakimbikizi hao waliokimbilia usalama wao.

Mapigano ya jana pekee yamekaribia eneo la Kambi ya Shimelba ambayo inawahifadhi takribani wakimbizi elfu sita mia tano kutoka Eritrea na hivyo kuibua hofu kuwa huenda wakimbizi wengine wakaitoroka kambi hiyo.

Kwa jumla mazingira ya UNHCR kuendesha operesheni zao ndani ya eneo la Tigray ni magumu kwa kuwa hakuna umeme na upatikanaji wa chakula.

Wakimbizi wengi wamekuwa wakivuka kupitia mpaka wa Hamdayet katika jimbo la Kassala na wengine katika kituo cha mpakani cha Ludgi katika jimbo la Gedaref.

Hayo yanajiri huku Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Nchini Sudan Kusini ukisema kuwa watu zaidi ya elfu moja wameuliwa huku mia nne wakitekwa nyara kufuatia mapigano nchini humo.

Kwa pamoja Umoja wa Mataifa umeendelea kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigani nchini Ethiopia vilevile Sudan Kusini na kuwaomba wahisani kuwasaidia wakimbizi na misaada ya kibinadamu.