
Shule ya Wasichana ya Oyugi Ogango katika Katika Kaunti ya Migori, inaombeleza kifo cha mwalimu mkuu Martha Ouma ambaye amefariki dunia mapema leo katika Hospitali ya Kisumu akitibiwa.
Wakazi, walimu, wanafunzi na wafanyakazi wamekongamana katika shule hiyo kuombeleza kifo chake.
Maafisa wa elimu wamepuuza taarifa kwamba amefariki dunia kutokana na Covid-19.
Mkurugenzi wa Elimu katika Kaunti ya Migori Elizabeth Otieno, amesema kifo cha Ouma ni pigo katika sekta ya elimu huku akiwaonyoa wanaosambaza uvumi kwamba amefariki kutona na Covid-19