
Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC sasa imemwalika Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwenye Kaunti ya Uasin Gishu Gitonga Mbaka kurekodi taarifa kuhusu kudhalilishwa kwake na Waziri wa Elimu George Magoha.
EACC imemuandikia Mbaka barua ikimtaka kushirikiana nao ili kufanikisha uchunguzi wao baada ya Magoha kunakiliwa kwenye video akimtusi Mkurugenzi huyo kutokana na hali mbovu ya shule ya Msingi ya Langas.
Kufuatia tukio hilo, Tume ya Huduma za Umma PSC, ilimpokonya Magoha mamlaka ya usimamizi wa wafanyakazi, hatua ambao Magoha aliipuuza akisema kwamba ataendelea na mfumo wake wa uongozi ambao anadai umeonesha kuzalisha matunda.