
Hatimaye Immaculate Kassait ameapishwa rasmi kuwa Kamishna wa Data katika hafla ambayo imefanyika katika Majengo ya Mahakama ya Juu na kuongozwa na Jaji Mkuu David Maraga.
Immaculate ambaye amekuwa Kamishna wa kwanza wa data ameanza majukumu yake rasmi leo hii.
Kassait aidha anatarajiwa kuanzisha utoaji wa kadi za Huduma Namba ambazo licha ya usajili kufanywa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, zimechukua muda kutolewa kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu wa kubuniwa kwa ofisi ya Kamishna wa Data.