×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mabunge ya kaunti yaonywa kuhusu siasa za BBI

Mabunge ya kaunti yaonywa kuhusu siasa za BBI

Mabunge ya kaunti hayapaswi kujihusisha katika siasa za kupinga au kuunga ripoti ya Mpango wa Upatanishi, BBI. Ndiyo kauli ya Naibu wa Rais, William Ruto.

Akihutubu baada ya kukutana na wawakilishi wadi wa Kaunti ya Wajir nyumbani kwake Mtaani Karen, Ruto badala yake amewataka kuungana na kufanya majadiliano ya kitaifa kuhusu BBI. Amerejelea kauli yake kwamba maoni ya kila mtu yanapaswa kuzingatiwa bila kuwabagua wengine hasa ikizingatiwa mianya iliyoko katika ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa Ruto, wanaopigia debe BBI bila kujumuisha maoni ya wenzao, wanafanya hivyo kujinufaisha, hali ambayo inatishia migawanyiko zaidi nchini.

Kwa upande wao wawakilishi wadi hao, wameapa kupinga BBI iwapo mapendekezo yalioibuliwa na Ruto hayatazingatiwa.

Wakati uo huo, Ruto ameongeza kwamba taifa linapaswa kufanya kipaumbele suala la afya ya watu wake wanaoathiriwa na janga la korona.

Jumapili wiki hii, Ruto alitaja korona kuwa hatari zaidi nchini na serikali inapaswa kuelekeza juhudi