×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 559 waambukizwa korona, 18 wakifariki dunia

Watu 559 waambukizwa korona, 18 wakifariki dunia

Mwezi huu umetajwa kuwa mbaya zaidi ambapo kufikia sasa watu  mia mbili sabini na wanne wamefariki kutokana na Covid19. Aidha sekta ya afya imeandelea kuathirika zaidi na awamu ya pili ya maambukizi ambapo kufikia sasa wahudumu wa afya thelathini wameaga dunia.

Watu kumi na wanane wamefariki katika saa ishirini na nne zilizopita huku mia tano hamsini na tisa wakiambukizwa.

Kenya ikiendelea kupambana na awamu ya pili ya maambukizi, chini ya siku kumi na tano pekee, watalamu wa fya wanane wamefariki dunia hii ikiwa pigo kwa taifa.

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amesema kuwa malalamiko ambayo yamekuwa yakiibuliwa na wahudumu wa afya yanashugulikiwa ikiwamo kupewa bima ya matibabu na vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi.

Ikumbukwe kwamba wahudumu wamekuwa wakilalamikia kutokuwa na bima miongoni mwa masuala mengine.

Kagwe amefanya mazungumzo na Kamati ya Kitaifa ya Kukabili Maambukizi ya Korona ambapo mikakati mipya ya kuzuia maambukizi mashinani imewekwa.

Haya yanajiri huku watu wengine mia tano hamsini na tisa wakiambukizwa korona kufuatia kupimwa kwa sampuli elfu tatu sabini na nne na hivyo basi kufikisha  elfu sabini, mia nane na nne.

Miongoni mwa walioambukizwa mia tano kumi na wanne ni Wakenya huku kumi na wanane wakiwa raia wa kigeni. Watu wengine mia nne sabini na wanane wapona  huku kumi na wane wakifariki dunia na kufikisha jumla ya vifo kuwa, elfu moja, mia mbili thelathini na saba.

Kaunti ya Nairobi imeendelea kuongoza kwa maambukizi mapya ambapo leo pekee watu arubaini na wawili wameambukizwa.

Kagwe aidha amesema kwamba  wimbi la pili la maambukizi limesababishwa na kupuuzwa kwa mwongozo wa kuzuia maambukizi hasa kufanyika kwa mikutano ya kisiasa.

Kuhusu chanjo ya korona amesema Kenya haitakimbilia chanjo yoyote  bali itasubiri kuona jinsia hali itakavyokuwa hasa kutokana na ugumu wa kuhifadhi chanjo hiyo.

Awali Kagwe alioneka kupinga chanjo mpya ya korona.