×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Malawi yaikashifu Afrika Kusini kwa kuchelewesha ndege ya rais Chakwera

Malawi yaikashifu Afrika Kusini kwa kuchelewesha ndege ya rais Chakwera

Serikali ya Malawi, imeendeleza shutma dhidi ya Afrika Kusini kufuatia kucheleweshwa kwa ndege iliyokuwa imsafirishe Rais Lazarus Chakwera kurejea Malawi.

Kupitia Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni, Malawi imesema kwamba rais Chakwera alipitia hali isiyostahili hadhi yake kabla ya ndege kuondoka.

Mzozo wa kidiplomasia umeibuka baina ya mataifa haya mawili baada ya Chakwera na ujumbe wake kuzuia kuondoka nchini humo .

Inadaiwa kwamba rais huyo alijaribu kuwasafirisha kinyume na sheria wakimbizi wawili raia wa taifa lake waliokuwa Afrika Kusini.

Hata hivyo, baadaye Serikali ya Afrika Kusini ilithibitishwa kwamba watu hao wawili hawakuwa katika msafara wa Chakwera.

Ndege yake imekuwa chini ya ungalizi mkali wa jeshi la Afrika Kusini katika Makao Makuu ya Jeshi ya Waterloof mjini Pretoria.