
Sasa ni rasmi kwamba shughuli za masomo kote nchini zitarejelewa tarehe 4 mwezi Januari mwaka ujao na muhula wa kwanza kukamilik atarehe 19 mwezi Machi.
Akitangaza haya, Waziri wa Elimu Prof. George Magoha amesema kwamba hili limeafikiwa kufuatia mkutano uliowaleta pamoja washikadau wa sekta ya elimu na wameafikiana kuhusu tarehe hiyo pamoja na kalenda nzima ya masomo ikiwemo tarehe za kufanya mitihani.
Kwa upande wake, Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Huduma kwa Walimu, TSC Nancy Masharia amewahakikishia walimu kwamba walimu wenye umri wa zaidi ya miaka 58 na zaidi hawatafutwa kazi jinsi imekuwa ikidaiwa na kwamba tayari mipango kabambe ipo kuhakikisha kwamba walimu wanaougua ugonjwa wa Covid-19 wanapokea matibabu kwa dharura.
Ikumbukwe kuwa Rais alitoa makataa ya siku 14 kwa Wizara ya Elimu kutoa kalenda ya jinsi masomo yatakavyorejelewa.