×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kagwe ataja wiki hii kuwa pigo kwa taifa kufuatia vifo vya madaktari wanne

Kagwe ataja wiki hii kuwa pigo kwa taifa kufuatia vifo vya madaktari wanne

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe ametaja wiki hii kuwa pigo kwa taifa kufuatia vifo vya madaktari wanne waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Kwa mujibu wa Kagwe, idadi ya vifo imeongezeka wiki hii tangu kuripotiwa kwa Janga la korona nchini humu.

Haya yanajiri huku Kagwe akiitisha mkutano wa dharura kesho ili kujadili kuhusu janga la korona nchini.

Wakati uo huo, Kagwe ametoa takwimu za leo kuhusu korona ambapo watu mia tisa sabini na wawili wameambukizwa virusi hivyo.

Idadi hii imetokana na sampuli elfu sita, mia sita arubaini na nane zilizopimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Maambukizi ya leo yamefikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa elfu sabini, mia mbili arubaini na matano.

Mia tisa ishirini na tisa miongoni mwao ni Wakenya, arubaini na watatu wakiwa raia wa kigeni. Mia tano themanini na watatu ni jinsia ya kiume huku mia tatu themanini na tisa wakiwa wa jinsia ya kike.

Pia mtoto wa miezi mitano na mkongwe wa miaka tisini na mmoja ni miongoni mwa walioambukizwa.

Kiwango cha maambukizi leo hii ni asilimia 14. 6 kulinganisha na jana ambapo kilikuwa asilimia 10.

Vilevile Watu mia tatu hamsini na wawili wamepona na kufikisha idadi ya waliopona nchini kuwa watu elfu arubaini na watano, mia saba sitini na sita.

Watu tisini na tisa walikuwa katika hospitali mbalimbali na wengine mia mbili hamsini na watatu ni wale waliokuwa wakihudumiwa nyumbani.

Cha kusikitisha ni kuwa watu ishirini wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya vifo nchini kuwa elfu moja, mia mbili sitini na sita.

Kulingana na Kagwe, watu wengine elfu moja, mia mbili ishirini na tisa wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini, elfu tano, mia tano sabini na wawili wakiwekwa karantini nyumbani.

Watu hamsini na tisa wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi, 26 wanatumia vipumuzi, 30 wako kwenye oxijeni huku 17 wakiwa wale wanaohitaji uangalizi wa karibu.

Share this: