×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wanaompinga Wetangula wakome-Peter Kaburu

Wanaompinga Wetangula wakome-Peter Kaburu

Mvutano ukiendelea kuhusu mkutano wa Ford Kenya tarehe 21 mwezi huu kumchagua kiongozi mpya wa chama hicho, wandani wa Seneta wa Bungoma Moses Wetangula wameapa kumchagua tena.

Katibu wa Ford Kenya kwenye Eneo la Cherang'any Peter Kaburu amewataka wandani wa Mbunge wa Kanduyi Wafula Wamunyinyi kuendeleza mipango ya kufanikisha mkutano huo katika ukumbi wa Bomas akisema wako tayari kushiriki uchaguzi huo na kumchagua Wetangula.

Aidha Mwenyekiti wa Ford Kenya katika Eneo Bunge la Kwanza Peter Puka na Antony Sikhulu wa Saboti ambao wanaegemea upande wa Wamunyinyi wamesema wakati umefika kwa wachama wa chama hicho kufanyia madiliko uongozi wa Ford Kenya, wakimshtumu Wetangula kwa kuahirisha uchaguzi huo mara kwa mara.

Ikumbukwe jana, Wafula Wamunyinyi alisisitiza kwamba mkutano huo ulioratibiwa kufanyika tarehe 21 mwezi huu utafanyika licha ya Wetangula kuupuzilia mbali.