
Mjadala ukiendelea nchini kuhusu Ripoti ya BBI Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Fred Matiangi amewataka viongozi kushauriana.
Akizungumza kwenye eneo la Egesenta katika Kaunti ya Kisii amewataka viongozi wa kisiasa kukomesha mijadala inayoibua migawanyiko kutumia BBI.
Amesema ni muhimu sana kwa viongozi kuzingatia masuala ya manufaa kwa Wakenya kwanza.
Kauli ya Matiangi, wakati ambapo Kiongozi wa Chama cha ODM Raila Odibnga anatrajiw akukutana na washikadau mbalimbali wiki hii kupanga mikakati kabla ya shughuli ya ukusanyaji saini kuanza.