×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

1065 waambukizwa korona, 10 wafariki

1065 waambukizwa korona, 10 wafariki

Idadi ya maambukizi nchini imefikia watu elfu sitini na moja, mia saba sitini na tisa baada ya watu wengine elfu moja na sitini na watano kuambukizwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Haya yanajiri baada ya sampuli elfu saba, mia tatu themanini na sita kupimwa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Afya imesema miongoni mwa waliopimwa, mia tisa tisini na watatu ni Wakenya huku sabini na wawili wakiwa raia wa kigeni.

Leo hii viwango vya maambukizi ni asilimia 14. 42 ikilinganishwa na jana ambayo ilikuwa asilimia 15. 5.

Aidha, watu mia sita sitini na mmoja ni wanaume, huku wanawake wakiwa mia nne na wanne. Mtoto mdogo wa miaka mitatu na mkongwe wa umri wa miaka mia moja na minne ni miongoni mwa waliambukizwa virusi vya korona.

Kaunti za Nairobi na Mombasa zimeripoti idadi ya juu zaidi ya maambukizi ambapo watu mia mbili sitini na watatu wameambukizwa hapa Nairobi, mia moja themanini na mmoja wakiambukizwa jijini Mombasa.

Taarifa hiyo pia inaashiria kwamba watu wengine mia nane themanini na wanane wamepona ugonjwa wa Covid-19 na kufikisha jumla ya waliopona nchini kuwa watu elfu arubaini na mmoja, na kumi na tisa.

Miongoni mwao, mia nane ishirini na wanne walikuwa wakihudumiwa nyumbani, sitini na wanne wakilazwa katika hospitali mbalimbali.

Hata hivyo, watu kumi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha jumla ya vifo kuwa elfu moja, mia moja na vitatu.

Hadi sasa, watu elfu moja mia mbili sabini wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini. Wengine elfu tano, mia tano thelathini na saba wamewekwa karantini nyumbani.

Hamsini na tisa wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi, ishirini na sita wakitumia vipumuzi, ishirini na saba wakitumia oxijeni na kumi na wanne wakiwa katika vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa kairibu.

Share this: