×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

16 wafariki dunia kutokana na COVID-19 Kenya

16 wafariki dunia kutokana na COVID-19 Kenya

Idadi ya watu wanaofariki dunia kutokana na COVID-19 inaendelea kuongezeka huku watu 16 wakiaga dunia katika kipindi cha saa 24.

Idadi hii inafikisha 858 idadi jumla ya waliofariki humu nchini.

Wagonjwa wa COVID-19 waliolazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi ni 27 ambao wamewekewa vipumuzi na wengine 41 wakihitaji usaidizi wa hewa ya oxygen.

Kwa jumla idadi ya walioalazwa katika hospitali mbalimbali nchini ni 1, 189.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema, watu 497 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Korona.

Idadi hii imetokana na sampuli 4, 888 zilizopimwa, kurekodi asilimia 10. 2 ya viwango vya maambukizi.

Watu 238  wamethibitishwa kupona na kufikisha idadi jumla kuwa 32, 760