×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta na Raila wapokea Ripoti ya Upatanishi

Rais Kenyatta na Raila wapokea Ripoti ya Upatanishi

Ripoti ya Pili ya Mpango wa Upatanishi BBI inapendekeza kubuniwa kwa wadhifa wa waziri mkuu na manaibu wake wawili ambao watakuwa chini ya rais. 

Miongoni mwa masuala makuu tisa yaliyopendekezwa, Waziri Mkuu na manaibu wake wawili watateuliwa na Rais kutoka bungeni wakiwa wabunge wa maeneo tofautitofauti.

Aidha, waziri mkuu atachaguliwa kutoka chama cha wabunge wengi, vilevile mawaziri wakipendekezwa kuteuliwa miongoni mwa wabunge.

Waziri Mkuu ataongoza shughuli za serikali katika Bunge la Kitaifa na kusimamia Vikao vya Baraza la Kitaifa la Usalama, huku Rais akiwa na mamlaka ya kumfuta kazi wakati wowote.

Vilevile, BBI inapendekeza kubuniwa kwa wadhifa wa kiongozi wa upinzani ambaye ni mgombea atakayeibuka wa pili katika kinyang'anyiro cha urais

Nyadhifa za kiongozi wa wengi na wa wachache zimeondolewa kwenye mabunge ya Kitaifa na Seneti, huku viongozi wawili ambao mmoja atakuwa wa kike na mwingine wa kiume wakipendekezwa kuchaguliwa kwa kila kaunti, ili kufanikisha uwakilishi wa kijinsia katika seneti.

Vilevile, Tume ya Huduma za Vijana imependekezwa kubuniwa.

Ili kudumisha ugatuzi, BBI imependekeza mgao wa fedha za kaunti kwenye Hazina ya Kitaifa kuongezwa kutoka asilimia kumi na tano hadi thelathini na tano. Vilevile magavana watatakiwa kuwateua manaibu wao kutoka miongoni mwa mawaziri wa kaunti.

Aidha, ripoti hiyo imependekeza Idara ya Mahakama kupewa uhuru zaidi na hata kubuniwa kwa Ofisi ya Tume ya Utawala wa Haki Ombudsman ya kuchunguza malalamishi ya wananchi