×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Tusitumie BBI kuwagawanya Wakenya, Rais Kenyatta asema

Tusitumie BBI kuwagawanya Wakenya, Rais Kenyatta asema

BBI hailengi kubuni wadhifa wa urais ama uwaziri mkuu kwa ajili ya mwanasiasa fulani.

Ndiyo kauli ya Rais Uhuru Kenyatta baada ya kupokea Ripoti ya Pili ya Mpango wa Upatanishi BBI, akiwa na Mshirika wake ambaye ni Kinara wa ODM Raila Odinga.

Akizungumza katika Ikulu Ndogo ya Kisii, Rais Kenyatta amekariri kwamba Mpango wa BBI haukulenga kumkandamiza mtu yeyote wala jamii bali ni nafasi ya kuwa na mazungumzo ya kuliendeleza taifa hili.

Katika kauli inayofikirika kumlenga Naibu wa Rais William Ruto na washirika wake ambao wamekuwa wakipinga BBI, Rais amewahimiza wanasiasa kukoma kuingiza siasa katika mpango huo.

Kauli sawa na hiyo imetolewa na Raila, ambaye amesema kwa sasa Wakenya wana fursa ya kujadili mapendekezo ya BBI kabla ya kuamua iwapo katiba itafanyiwa marekebisho au la.

Ametumia nafasi hiyo kuendelea kumkashifu Ruto ambaye amekuwa akikosoa jinsi BBI imekuwa ikishughulikiwa kwa kuwatenga viongozi wengine.

Rais na Raila wamepokezwa ripoti hiyo na Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kushughulikia Mpango wa BBI, Adams Oloo

Wakati uo huo, Rais Kenyatta amesema jukumu kuu la kamati ya BBI lilikuwa kuitayarisha ripoti ya kwanza kuwa katika lugha ya kisheria, ili kutumika kubuni hoja ya kura ya maamuzi.

Amesema ana imani BBI itawaunganisha Wakenya, na kwamba hakuna uhasama utakaoshuhudiwa tena wakati wa uchaguzi.

Aidha, Kenyatta amewataka Wakenya kujisomea mapendekezo ya BBI bila kuwazia miegemeo ya kisiasa.

Kamati ya BBI sasa imeagizwa kusambaza ripoti hiyo kwa kila Mkenya, huku vikao vya kwanza vya kujadili ripoti hiyo vikitarajiwa kufanyika Jumatatu ijayo katika Ukumbi wa Bomas, Nairobi.