×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais na Mkewe wapata kadi za Huduma Nanda

Rais na Mkewe wapata kadi za Huduma Nanda

Wakenya wametakiwa kujitayarisha kuanza kupokea kadi zao za huduma Namba baada ya sampuli ya kadi hizo kuzinduliwa rasmi katika maadhimisho ya Mashujaa.

Rais Uhuru Kenyatta na mkewe Bi Margaret Kenyatta wamekuwa wa kwanza kupokezwa rasmi  sampuli ya kadi ya Huduma Namba, kuashiria kukamilika kwa shughuli ya  utengenezaji wa kadi hizo.

Akizungumza baada tu ya Rais Uhuru Kenyatta kumaliza hotuba yake, Waziri wa Masuala ya Ndani na Usalama Dkt Fred Matiang'i  amesema kinachosubiriwa  sasa ni bunge kupitisha  jina la Immaculate Kassait kuwa kamishna wa data, shughuli inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo ili kupisha utoaji wa kadi hizo.

Rais Kenyatta pia amewakabidhi Wakenya kadhaa sampuli za kadi hizo.