×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Uhuru Kenyatta ametumia mfano wa uongozi wa mashujaa kupigia debe marekebisho ya katiba kupitiam BBI

Rais Uhuru Kenyatta ametumia mfano wa uongozi wa mashujaa kupigia debe marekebisho ya katiba kupitiam BBI

Suala la katiba kufanyiwa marekebisho limetawala hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa katika uwanja wa Gusii kwenye Kaunti ya Kisii.

Rais aidha ametoa wito wa kujenga moyo kubadili katiba panapokuwa haja.

Katika hotuba yake Rais Kenyatta aidha amesisitiza haja ya Wakenya kutambua jinsi ambavyo Kenya imekuwa ikipoteza muda wa takribani miaka miwili kushugulia masuala ya uchaguzi kila baada ya changuzi kuu zinapofanyika.

Vilevile Rais amesema marekebisho hayo yatondoa ushindani na migawanyiko ya kisiasa yanayokwamisha maendeleo.

Kenyatta amesema kupitia marekebisho hayo baishara zitazidi kuimarisha nataifakukua kiuchumi.

Kwenye hotuba hiyo ambayo hata hivyo Rais amekosa kutambua uwepo wa Jaji Mkuu David Maraga, Kenyatta aidha amehimiza kuendelea kutambuliwa kwa vijana wakati huu wa sherehe ya mashujaa kutokana na juhudi zao za ujenzi wa taifa. Ametoa mfano wa Japhet Shamala ambaye alihusika katika kuandaa sheria za uongozi wataifahili wakati wa ukoloni.