×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Maambukizi ya Korona yaendelea Kuongezeka Kenya

Maambukizi ya Korona yaendelea Kuongezeka Kenya

Kiwango cha maambukizi ya Korona nchini Kenya kimepanda na kufikia asilimia 14 baada ya watu wengine 571 kupatikana na virusi vya Korona kutoka sampuli 3963 zilizopimwa katika saa 24.

Mkondo wa maambukizi umesalia juu ya asilimia 10 kwa kipindi cha wiki moja sasa.

Idadi ya walioambukizwa Korona sasa ni 45 , 000 huku idadi ya waliolazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi ikifika 43 baada ya 39 ya siku iliyotangulia.

Walio katika mishine ya Oksijeni ni 41 huku kwa jumla  kukiwa na wagonjwa 1, 059 waliolazwa huku wengine wakitibiwa nyumbani.

Katika takwimu za 20/20/2020, maambukizi yameenea zaidi katika kaunti baada ya kuripotiwa watu 116 katika Kaunti ya Uasin Gishu sawa na Nairobi. Kaunti za Mombasa, Kiambu, Laikipia, Kericho, Kisumu, na Nakuru zinafuatia.

Hata hivyo watu 438 wamepona, 373 miongoni wakiwa nyumbani. Watu wengine watatu wameaga dunia na kufikishsha 842 idadi ya watu walioaga dunia.

Share this: