×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakenya Washerehekea Mashujaa Day katika mazingira tofauti

Wakenya Washerehekea Mashujaa Day katika mazingira tofauti

Rais Uhuru Kenyatta anawaongoza Wakenya kuadhimisha siku kuu ya kitaifa ya Mashujaa Day katika kaunti ya Kisii.

Kabla ya kuitwa Mashujaa Day ili kuwasherehekea mashujaa wote baada ya katiba kufanyiwa marekebisho mwaka wa 2010, siku hii awali iliitwa Kenyatta Day tangu Oktoba mwaka wa 1963,  kwa ukumbusho wa Rais wa Kwanza wa Taifa hili Hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Hayati Mzee Kenyatta, alishirikiana na mashujaa wenzake watano maarufu Kapenguria Six, ambao ni marehemu Achieng' Oneko, Bildad Kaggia, Kung'u Karumba, Fred Kubai, na Paul Ngei waliokuwa wa kundi la Mau Mau ili kuwatimua Wakoloni nchini.

Maadhimisho ya leo ni ya tano kufanyika nje ya Nairobi kwani 2019 yalifanyikia Mombasa, baada ya Rais Kenyatta mwaka 2015, kuidhinisha hafla za siku kuu za kitaifa kufanyika katika kaunti mbalimbali kuanzia mwaka wa 2016.

Hafla hii inafanyika katika mazingira tofauti kabisa na miaka ya awali, kufuatia Janga la Korona chini ya masharti makali ya kuzuia maambukizi ya Virusi vya Korona.

Leo Wakenya hawatakuwa na fursa ya kujaa uwanjani ili kupiga kelele za kushangilia majina ya mashujaa mbalimbali yakitajwa.

Watu elfu nne wamealikwa kuingia katika Uwanja wa Gusii, licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kustahimili wingi wa watu elfu ishirini na tano.

Vilevile,  zaidi ya runinga kumi na tano zimewekwa katika maeneo mbalimbali mjini Kisii, ikiwamo nje ya Uwanja wa Gusii, Kisii Golf Club na katika Shule ya Msingi ya Kisii ili kuwawezesha wananchi kufuatilia maadhimisho hayo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama Karanja Kibicho, huenda ratiba ya shughuli za maadhimisho hayo ikabadilika kutokana  na masharti makali yaliyowekwa.

Miongoni mwa shughuli ambazo huenda zikakosa kufanyika, ni gwaride la maskauti hasa watoto na polisi wa utawala ambao hushiriki katika tamasha za kupamba siku kama ya hii.